pmbet

Utaishia kama Saddam, Israel yamtisha Rais wa Uturuki

Eric Buyanza

July 29, 2024
Share :

Israel imemuonya Rais Erdogan wa Uturuki kwamba hatima yake itaishia kuwa kama ya Saddam Hussein, hii ni baada Rais huyo wa Uturuki kutishia kuwa nchi yake inaweza kuivamia Israel na kutuma vikosi vyake kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel.

"Lazima tuwe thabiti ili Israeli isiweze kufanya mambo haya kwa Palestina," alisema Erdogan, akimaanisha mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza.

"Kama tulivyoingia Nagorno-Karabakh na tulivyoingia Libya, tunaweza kuwafanyia vivyo hivyo Israel. Hakuna kitu ambacho hatuwezi kufanya."

Mara tu baada ya kauli hiyo ya Erdogan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, kupitia ukurasa wake wa X alimuonya rais huyo wa Uturuki kwamba akijaribu kufanya hicho anachofikiri basi yatamkuta kama yaliyomkuta Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet