Utambulisho wa Mourinho Fenerbahce wajaza Uwanja
Sisti Herman
June 3, 2024
Share :
Maelfu ya mashabiki wa klabu ya Fenerbahce jana walijitokeza katika mapokezi ya kocha wao mpya, Jose Mourinho wakati akitambuliwa kwenye Uwanja wa Sukru Saracoglu Jijini la Istanbul, leo Juni 2, 2024
Kocha huyo amerejea katika majukumu hayo ikiwa ni miezi mitano tangu alipofukuzwa katika Klabu ya Roma ya Italia. Baada ya kutambulishwa akiwa na jezi ya Fenerbahce, Mourinho amesema “Hii jezi sasa ni ngozi yangu, ndoto zenu ni ndoto zangu”
Mourinho (61) ambaye alianza Majukumu ya kuwa Kocha Mkuu Mwaka 2000, ameshazitumikia Benfica, Uniao de Leiria, Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Manchester United, Tottenham Hotspur na Roma