pmbet

Utata waibuka baada ya kifo cha Askari kufia mahabusu.

Joyce Shedrack

September 1, 2026
Share :

Kifo cha askari wa Jeshi la Polisi, Koplo Mwita Mrumbe, mwenye namba H.1796, kimeibua sintofahamu kuhusu mazingira ya kifo chake, huku Polisi Mkoa wa Tanga likisema amefariki dunia akiwa mahabusu.

Mwili wa Koplo Mwita umezikwa jana Jumatatu Agosti 31, 2026, saa tisa alasiri, katika makaburi ya Mwanagati, Ilala jijini Dar es Salaam, siku nne baada ya kufariki akiwa katika kituo cha Polisi Wilaya ya Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Mwita alifariki dunia Agosti 27, 2026 saa 1:03 usiku, akiwa ndani ya chumba cha mahabusu katika kituo hicho.

Taarifa hiyo inaeleza kabla ya kifo chake, Mwita pamoja na ofisa mmoja na askari watano wa Jeshi la Polisi wenye vyeo mbalimbali, walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai.

"Marehemu, pamoja na ofisa mmoja na askari watano wa Jeshi la Polisi wa vyeo mbalimbali, walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai."

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uchunguzi wa kisayansi uliofanyika huku ndugu wa marehemu wakishuhudia, umebaini kuwa chanzo cha kifo chake ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limewataka wananchi, baadhi ya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa au kutoa hitimisho lisilotokana na matokeo rasmi ya uchunguzi. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kukamilishwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kiuchunguzi.

 


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet