Utawala Burkina Faso wapiga marufuku ushoga
Eric Buyanza
July 11, 2024
Share :
Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso umeidhinisha muswada wa kupiga marufuku ushoga, hatua inayolifanya kuwa moja ya mataifa ya Afrika kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa ofisi ya rais, mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika siku ya Jumatano ya wiki hii uliidhinisha mpango huo unaopiga marufuku ushoga.
Bila ya kuweka wazi adhabu itakayotolewa kwa wahusika wa vitendo hivyo, Waziri wa Sheria Edasso Rodrigue Bayala alieleza kuwa ushoga na vitendo vinavyohusiana na mambo kama hayo vitaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
RFI imeripoti kuwa muswada huo unatarajiwa kuwa sheria baada ya kuidhinishwa na wabunge katika bunge la mpito ambalo limekuwa likitumika tangu kutokea kwa mapinduzi mawili ya kijeshi.