Uturuki waandamana kupinga mashambulizi Gaza
Sisti Herman
January 1, 2024
Share :
Mamia kwa maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano leo tarehe 1 Januari jijini Istanbul, Uturuki kuunga mkono Wapalestina wakati mashambulizi ya Israeli yakiendelea Gaza.
Waandamanaji hao pia, wamelaani shambulio la PKK ambalo liliuwa wanajeshi 12 wa Uturuki kaskazini mwa Iraq wiki kadhaa zilizopita.