Uturuki yabadilisha jina la mtaa kwa heshima ya Mohamed Salah
Eric Buyanza
August 31, 2026
Share :

Manispaa ya Yomra iliyopo mkoani Trabzon nchini Uturuki imechukua hatua ya kubadilisha jina la mtaa anaoishi Mohamed Salah na kuuita 'Mtaa wa Mohamed Salah' kama sehemu ya kumpa heshima ya kipekee.
Mtaa huo unaojulikana sasa kama "Selvi Sokak" uliopo katika Kata ya Kaşüstü, unatarajiwa kubadilishwa jina wiki hii baada ya kikao cha Baraza la Manispaa.
Meya wa Yomra, Mustafa Bıyık, alithibitisha hatua hiyo kupitia mitandao ya kijamii na kueleza kuwa ujio wa Salah ni tukio kubwa la kihistoria.
"Tuna jambo kubwa la kujivunia kwamba Mohamed Salah, ambaye ni usajili mkubwa zaidi katika historia ya soka la Uturuki, atakuwa akiishi katika wilaya yetu," alisema Meya Bıyık. "Kupitia uamuzi wa baraza tutakaoufanya wiki hii, tutaupa mtaa uliopo nyumba yake jina la 'Mtaa wa Mohamed Salah.' Sisi tumefanya sehemu yetu, sasa ni zamu ya Salah" alisema.
Meya huyo aliongeza kuwa kuwepo kwa staa huyo wa kimataifa wilayani humo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupandisha thamani ya eneo hilo duniani kote.





