Uwanja mpya wa Man Utd kuingiza mashabiki laki 1
Sisti Herman
July 31, 2024
Share :
Mabosi wapya wa klabu ya Manchester United kamouni ya INEOS chini ya Mkurugenzi Sir Jim Ractliffe wamepitisha mpango wa kujenga uwanja mpya utakaobeba mashabiki laki moja (100,000) huku Uongozi wa klabu hiyo ukiamini kujenga uwanja mpya kutakuwa na manufaa zaidi kuliko kukarabati uwanja uliopo wa sasa wa Old Trafford ambao unahitaji maboresho makubwa.
Mipango ambayo ipo hadi sasa ni kuwa ujenzi wa uwanja huo mpya utakamilika ifikapo 2030, huku mradi huo ukikadiriwa kugharimu Euro bilioni 2.4 (Trilioni 69).