Uwanja mpya wa Yanga kukamilika ndani ya miezi 18 hadi 24 ijayo.
Joyce Shedrack
May 15, 2026
Share :
Klabu ya Yanga imefanya hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa uwanja wao utakaojengwa maeneo ya Jangwani ndani ya miezi 18 hadi miezi 24 ijayo.

“Matarajio yetu ni kwamba ujenzi wa uwanja huu utakuwa umekamilika na kuzinduliwa rasmi ndani ya kipindi cha miezi 18 hadi 20 ijayo. Tuna imani na matumaini makubwa kwamba mradi huu utakamilika kwa wakati uliopangwa na kuwa sehemu muhimu ya historia ya klabu yetu.
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mara nyingine kwa Ghalib Said Mohamed pamoja na familia yake, kwa maamuzi yao makubwa na ya kizalendo waliyochukua kwa ajili ya kusaidia kutimiza ndoto ya muda mrefu ya Young Africans S.C.” Amesema Rais wa Yanga Eng. Hersi Ally Said





