Uwanja mpya wamtamanisha Klopp kurudi kwenye ukocha
Eric Buyanza
April 24, 2026
Share :

Kocha wa zamani wa Liverpool, Jürgen Klopp amesema uwanja mpya wa mazoezi wa timu ya New York Red Bulls ni mzuri sana kiasi kwamba ulikaribia kumfanya atamani kurejea kwenye ukocha.
Klopp alijiuzulu nafasi yake kama kocha wa Liverpool msimu wa joto wa 2024 na hajafundisha tangu wakati huo. Hivi majuzi alihusishwa na kuchukua mikoba ya kuinoa Real Madrid msimu huu wa joto, lakini alipuuzilia mbali uvumi huo na kuuita "upuuzi".
New York Red Bulls ni moja ya vilabu kadhaa vinavyomilikiwa na chapa ya kinywaji cha kuongeza nguvu ambacho Klopp anasaidia kusimamia akiwa kama mkuu wa idara ya soka ya timu za Red Bull duniani, aliteuliwa kushika wadhifa huo Januari 2025.





