Uwanja wa AFCON Arusha wafikia asilimia 74 za ujenzi.
Joyce Shedrack
January 31, 2026
Share :
Ujenzi wa uwanja unaotarajiwa kutumika kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027 unaojengwa Jijini Arusha umefikia asilimia 74% hadi sasa ili kukamilika.

Uwanja huo unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu (2026) na utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 32,000, ukiwa umejengwa kwa hadhi ya kiwango cha juu kabisa kinachotambuliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).





