pmbet

Uwanja wa Yanga kumilikiwa asilimia 50 na Yanga na 50 na GSM.

Joyce Shedrack

May 15, 2026
Share :

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha kuwa uwanja wa klabu hiyo unaotarajia kujengwa Jangwani utakuwa na umiliki wa asilimia 50 kwa Yanga na asilimia 50 kwa GSM.

“Nathibitisha rasmi leo kuwa Young Africans S.C. imeingia katika makubaliano ya ubia wa umiliki wa uwanja wetu mpya kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50 na GSM Group.

Tunamshukuru kwa dhati Ghalib Said Mohamed kwa moyo wake wa kizalendo na uamuzi wake wa kuweka usawa katika umiliki wa mradi huu mkubwa, licha ya kuwa yeye ndiye anayechangia sehemu kubwa zaidi ya uwekezaji wa kifedha.

Kwa upande wa klabu, Young Africans S.C. itatoa ardhi kwa ajili ya mradi huo, huku mchango wa GSM Group ukiwa ni uwekezaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo wa kisasa.” Eng. Hersi Ally Said

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet