UZEE DAWA: Kane atajwa kuwa 'Center Forward' bora zaidi duniani
Eric Buyanza
August 20, 2026
Share :

ESPN imemtambua Harry Kane kama mshambuliaji wa kati (center forward) bora zaidi duniani kwa sasa. Kupitia orodha yao maarufu ya kila mwaka ya ESPN FC 100 ya mwaka 2026, nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza na mshambuliaji wa Bayern Munich ameshika nafasi ya kwanza (#1)
Kane amefanikiwa kuwagaragaza mastaa wakubwa duniani ambao wameingia kwenye watatu bora nyuma yake.
ESPN wameeleza kuwa Kane sio tu mfungaji wa mabao, bali uwezo wake wa kushuka chini kabisa (deep), kutengeneza nafasi za mabao kwa wachezaji wenzake, na kuunganisha timu unamfanya kuwa mshambuliaji aliyekamilika zaidi duniani.
Katika msimu uliopita, akiwa na Bayern Munich, alifunga jumla ya mabao 61 na kutoa pasi za mabao (assists) 7 katika michezo 51 tu aliyocheza kwenye mashindano yote.
Licha ya kuwa na umri wa miaka 33, wachambuzi wa ESPN wamebainisha kuwa tofauti na Mbappé na Haaland wanaotegemea zaidi kasi na nguvu za miili yao, Kane anatumia zaidi akili kubwa ya mpira, mbinu, na usomaji wa mchezo uwanjani.
Hii hapa orodha ya 10 bora;
1. Harry Kane
2. Kylian Mbappé
3. Erling Haaland
4. Ousmane Dembele
5. Julián Álvarez
4. Ousmane Dembélé
5. Julián Alvarez
6. Lautaro Martínez
7. Kai Havertz
8. João Pedro
9. Victor Osimhen
10. Hugo Ekitiké
Je, unakubaliana na orodha hii?





