V8 yakamatwa na polisi ikisafirisha wahamiaji haramu
Eric Buyanza
April 8, 2024
Share :
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewakamata watu 17 ambao ni raia wa Ethiopia, kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kutokuwa na vibali.
Akitoa taarifa hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Lucas Mwakatundu, ameeleza kuwa watu hao wamekamatwa katika Kijiji cha Kiongozi, kilichopo wilayani Babati, wakisafirishwa kwenye gari aina ya V8 VXR yenye namba bandia za serikali, STL 1964, huku dereva wa gari hilo akikimbia baada ya kugundua kuwa anafuatiliwa na Polisi.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, limewaomba wananchi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Polisi ili kuhakikisha hakuna magendo yanayopitishwa kwa kutoa taarifa za watuhumiwa wa uhalifu.