pmbet

Van Nestelrooy aanza na ushindi Leicester

Sisti Herman

December 4, 2024
Share :

 

Ruud Van Nistelrooy ameendelea kufanya maajabu kwenye kazi yake ya ukocha baada ya kuiongoza Leicester City kushinda 3-1 dhidi ya Wagonga nyundo, West Ham United kwenye mechi yake ya kwanza kama kocha mkuu mpya ya klabu ya Leicester City.

Van Nistelrooy alifanya vizuri akiwa kocha wa muda wa Manchester United kufuatia kutimuliwa kwa Erik Ten Hag akiwaongoza Mashetani hao Wekundu kwenye mechi nne akishinda tatu na kutoka sare mchezo mmoja kabla ya Ruben Amorim kushika hatamu.

Mpaka sasa Van Nistelrooy hajapoteza mechi yoyote kwenye Ligi Kuu England ambapo kwenye mechi 5 akiwa kocha ameshinda nne na kutoka sare mchezo mmoja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet