Van Nistelrooy awasili mazoezini kuanza kazi Man Utd
Eric Buyanza
July 8, 2024
Share :
Mshambuliaji wa zamani Manchester United na timu ya Taifa ya Uholanzi, Ruud van Nistelrooy, amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington ikiwa ni siku ya kwanza ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.
United imewaajiri Van Nistelrooy na Rene Hake kama makocha wasaidizi chini ya Erik ten Hag.
Man U itathibitisha rasmi uwepo wao (kikazi) klabuni hapo mara tu vibali vyao vya kufanya kazi vitakapotoka.
Nistelrooy amerudi tena klabuni hapo baada ya miaka 18, itakumbukwa nguli huyu aliichezea Man U toka mwaka 2001 mpaka 2006.