Van Persie amtetea Raheem Sterling
Eric Buyanza
February 28, 2026
Share :
Kocha wa Feyenoord Robin van Persie, amejitokeza kumtetea Raheem Sterling baada ya kusemwa sana kutokana na kuonyesha kiwango hafifu kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye klabu hiyo.
Sterling alicheza dakika 30 kwenye mechi ya Feyenoord dhidi ya Telstar, lakini haukuwa mchezo mzuri kwake.
Van Persie ameeleza kuwa ukosoaji huo haukuwa na msingi, akisema, "Kwa vyovyote vile, alicheza dakika 30 tu baada ya miezi sita bila kucheza mechi rasmi. Tunazungumzia mchezaji bora ambaye ameshinda karibu kila kitu. Lakini kumkataa kwa kucheza nusu saa tu... utakuwa hauna unachokijua" alisema Persie huku akisisitiza kuwa ukosoaji huo ni wa kipuuzi kwa kuwa Sterling anajitafuta kurejesha upya kiwango chake.
Sterling, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Uholanzi mapema mwezi huu baada ya kukubaliana kusitisha mkataba wake wa pauni 325,000 kwa wiki na Chelsea mwezi Januari.






