Van Persie awa kocha mkuu wa timu ya ligi kuu Uholanzi
Sisti Herman
May 17, 2024
Share :
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Arsenal na Feyenoord Robin Van Pesrie ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Heerenveen ya ligi kuu Uholanzi.
Van Persie ambaye kabla ya hapo alikuwa kocha wa timu ya vijana ya Feyenoord anachukua mikoba ya timu hiyo ambayo ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo imebakiza mechi 1 kumalizika.