VAR yaziingiza kwenye mgogoro Wizara ya michezo na Shirikisho la soka
Sisti Herman
August 24, 2026
Share :

Waziri wa michezo wa Afrika kusini Gayton McKenzie amelitaka Shirikisho la soka nchini humo (SAFA) irejeshe kiasi cha pesa Randi milioni 13 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya matumizi ya teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR) ambayo haijaanza kutumika hadi sasa.
Waziri huyo pia amesema amekatishwa tamaa kwa sababu, akiwa Waziri, kuna mipaka ya kile anachoweza kufanya ndiyo maana hadi sasa imekuwa ngumu yeye kuchukua hatua zozote bila kuathiri utendaji wa mamlaka za soka.
“Tulipaswa kuwa na VAR.”
Sasa McKenzie ameiachia SAFA jukumu la kuchukua hatua.





