Varane apewa 'THANK YOU' Man Utd
Sisti Herman
May 14, 2024
Share :
Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa beki wao wa kati Raphael Varane ataondoka mwishoni mwa msimu huu wa 2023/24.
Varane anaondoka baada ya kuitumikia kwa misimu mitatu akitokea kwa mabingwa wa kihistoria wa UEFA Champions league, Real Madrid.
Varane anakuwa mchezaji wa Kwanza kuondoka msimu huu akipitiwa na fagio la wamiliki wapya wa klabu hiyo INEOS chini ya tajiri wa Kingereza Sir Jim Ratcliffe.