Vardy anaondoka Leicester City baada ya misimu 13
Sisti Herman
April 24, 2025
Share :
Klabu ya Leicester City imethibitisha kuwa nahodha wao na mshambuliaji wao bora Jamie Vardy ataondoka mwishoni msimu huu baada ya mkataba wake kutamatika.
Akiwa na Leicester City, nahodha huyo amekuwa sehemu ya kizazi cha dhahabu kilichoshinda Ubingwa wa Ligi kuu Uingereza, kombe la FA, Ubingwa wa ligi daraja la kwanza mara 2 na Ngao ya Jamii.
Vardy aliyedumu Leicester kwa misimu 13 akitokea Fleetwood kwa ada ya uhamisho ya Euro Milioni 1.