Victor Osimhen atajwa kuwa 'Baba wa soka la Uturuki'
Eric Buyanza
October 31, 2026
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa Galatasaray, Ümit Karan, amemtaja nyota wa kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen, kama "Baba" wa Ligi Kuu ya Uturuki (Süper Lig), kufuatia kiwango chake bora na ukomavu mkubwa wa kiakili aliouonesha uwanjani.
Karan alitoa kauli hiyo baada ya ushindi mnono wa Galatasaray wa mabao 4-0 dhidi ya Konyaspor ugenini siku ya Ijumaa, mchezo ambao Osimhen na mchezaji mwenzake Rafael Leão walicheka na nyavu.
Sifa hizo kutoka kwa mshambuliaji huyo wa zamani hazikuja tu kwa sababu ya uwezo wa Osimhen wa kufunga mabao, bali kutokana na uamuzi wake wa kiungwana wa kumuachia mchezaji mwenzake Rafael Leão apige mkwaju wa penati wakati wa mchezo huo.
Kitendo hicho kiliwashangaza wengi kwani muda huu Osimhen yuko kwenye mapambano ya kukifukuzia kiatu cha mfungaji bora wa ligi hiyo, lakini aliweka ubinafsi pembeni na kuamua kuweka mbele maslahi ya timu hiyo.
Kwa mujibu wa taratibu au tuite mipango ya ndani ya timu , Victor Osimhen ndiye mpiga penati mkuu na chaguo la kwanza la Galatasaray.





