(VIDEO) Ifahamu 'Meet us' Couple inayosumbua mitandaoni
Eric Buyanza
January 12, 2024
Share :
Rahim na Kendy ni couple iliyojizolea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ikifahamika zaidi kama “meet us” wamesema walikutana Instagram na mahusiano yalianza kwa urafiki wa kawaida kabla ya Rahim kufunguka kwa mrembo huyo na kuanza mahusiano ya kimapenzi rasmi.
Rahim na Kendy ni wazaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro japo kwa sasa wote wanaishi jijini Dar es Salaam na ni couple na inayopendwa zaidi na wafuasi wa mitandao ya Instagram na Tiktok kutokana na video wanazojirekodi wakiwa pamoja na kuzichapisha kwenye kurasa zao za mitandao hiyo.
PMTV imewatafuta na kufanya nao mahojiano na miongoni mwa mambo waliyosema ni kuwa wana furahia wanachokifanya kwani ndio uhalisia wa Maisha yao na mara nyingi kurekodi video inakuwa njia ya kuwapatanisha pale wanapokuwa na migogoro kwani kuna wakati huwa wanagombana, hata hivyo wawili hao wameweka wazi kwamba mwaka huu yaani 2024 wanatarajia kufunga ndoa.
Na Loyce Shedrack
TAZAMA MAHOJIANO YAO KWENYE VIDEO HAPO CHINI