(VIDEO) "Nililetewa mgao wangu, nikaurudisha" - Jerry Slaa
Eric Buyanza
December 22, 2023
Share :
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe Jerry Slaa amekemea ongezeko na utitiri wa vituo vya mafuta kwenye makazi ya watu bila kufuata taratibu na sheria za mipango miji.
Mhe Jerry Slaa, amekemea utitiri huo na kusema kuwa kazi ya kwanza atakayoanza nayo kesho ni kuanza kujitenga na uwepo wa utitiri wa vituo vya mafuta kwenye makazi ya watu ili kudhibiti ongezeko la vituo hivyo.
"Vituo vya mafuta vinajengwa kiholela, ukiuliza unaambiwa ni kanuni zilizopo, mbaya zaidi vituo vya mafuta vingine viko maeneo ya shule...hakuna utaratibu na wakati mwingine rushwa inatembea hadi kwa Waziri " amesena Jerry.
"Siku moja na mimi nikaletewa mgao wangu, nikauliza kwanini?...eti mgao wako na kwa kweli nilirudisha hiyo pesa kwa muhusika" ameongeza Jerry Slaa.
Hayo yemejiri leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wake na wanahabari ikiwa nisiku 100 tangu kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo na Rais Samia.
Aidha Waziri Jerry ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi.
Akihitimisha Mkutano huo Waziri Jerry amezuia wenyeviti wa serikali za mitaa kuuza ardhi za wananchi na badala yake uuzwaji wa ardhi utafanywa na maofisa wa ardhi wa manispaa.
(Habari na Loyce Obongo)