Video Support kuanza kutumika ligi kuu msimu ujao.
Joyce Shedrack
July 30, 2026
Share :
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema maandalizi ya kuanza kutumia mfumo wa Video Support (VS) katika Ligi Kuu ya NBC yako katika hatua za mwisho yakifikia zaidi ya asilimia 75.
Karia amesema TFF imefikia makubaliano na kampuni kutoka Ureno iliyopendekezwa na FIFA na CAF, ambapo wataalamu wake wanatarajiwa kuwasili nchini kwa ajili ya kusaini hati ya makubaliano, kufunga vifaa pamoja na kutoa mafunzo kwa waamuzi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
"Msimu ujao tutatumia Video Support (VS) badala ya VAR, Video Support (VS) inatoa nafasi kwa Kocha kuomba tukio lirudiwe ni lazima mwamuzi akubali na zipo nafasi nne kwa kila timu kuomba kurudiwa kwa tukio, tutatoa elimu kwa makocha ya namna anaweza kuomba tukio kurudiwa."- @wallacekaria Rais wa TFF.





