Video ya komasava yapasua mawingu...!Masaa 15 watazamaji milioni 1.
Joyce Shedrack
July 26, 2024
Share :
Video ya Komasava remix ya staa wa bongofleva Diamond Patnumz aliyowashirikisha Wakimataifa akiwepo msanii wa Marekani Jason Derulo na Waafrika Kusini Khalil Harisson pamoja na Chley Nkosi imefikisha watazamaji milioni 1 YouTube ikiwa yamepita masaa 15 pekee toka iachiwe.
Siku ya jana video remix hiyo ya ngoma ya Komasava iliyotikisa duniani kote iliingia namba moja 1 on Trending yakiwa yamepita masaa ya 3 tu baada ya kuachiwa.
Ikumbukwe, siku ya jana msanii Marioo aliachia video ya wimbo wake wa Hakuna Matata ambao ulikaa namba 1 on Trending kabla ya kuja kushushwa na video remix ya Komasava ya staa wa bongofleva nchini.
Kwasasa ngoma ya Marioo ina watazamaji laki 377 ikiwa namba mbili on Trending nyuma ya Komosava yenye watazamaji milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.