Vigogo wa Sudan wajimilikisha ligi ya Rwanda.
Joyce Shedrack
February 26, 2026
Share :
Klabu za Sudan Al Hilal Omdurman na Al Merrikh SC zinaongoza msimamo wa ligi kuu Nchini Rwanda mmoja akiwa nafasi ya kwanza na mwingine ya nafasi ya pili.
Klabu hizo mbili zinashiriki ligi hiyo kufuatia ombi lao kwa shirikisho la soka la Rwanda (FERWAFA) kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea Sudan.
Al Hilal wanaongoza ligi hiyo wakiwa na jumla ya alama 42 ikiongoza msimamo huo wenye kushirikisha jumla ya timu 18 huku Al Merrikh ikiwa na alama 40 ikiwa nyuma ya Al Hilal.





