Viingilio Kariakoo Derby hivi hapa, buku 5 tu unamuona Chama na Pacome
Sisti Herman
April 14, 2024
Share :
Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara imetaja viingilio rasmi vya mechi ya ligi kuu Tanzania bara itakayowakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba Aprili 20 kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam huku kiingilio cha chini kikiwa Tsh 5,000 tu.
Viingilio vya Kariakoo Derby;
VIP A 50,000/-
VIP B 30,000/-
VIP C 20,000/-
Machungwa 10,000/-
Mzunguko 5,000/-
Unakosaje kwa mfano?