Vijana 65,000 wahitimu mafunzo ya uzalendo Burkina Faso
Sisti Herman
August 29, 2026
Share :

Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traore, amehudhuria hafla ya kuhitimu kwa vijana 65,000 waliomaliza mafunzo ya lazima ya uzalendo nchini humo, huku akiwahimiza kufanya kazi kwa bidii ili kulinda uhuru na mshikamano wa taifa.
Serikali ya Traore ilianzisha mpango wa Mafunzo ya Lazima ya Uzalendo mwaka 2025, unaowataka wanafunzi wanaomaliza shule za sekondari kuhudhuria mafunzo ya mwezi mmoja yanayolenga kuwafunza maadili, uzalendo, nidhamu na uelewa wa historia. Baada ya mafunzo hayo, hupewa cheti ambacho ni sharti kwa ajili ya kujiunga na chuo kikuu.
“Mtu asiye na uelewa ni hatari kwa mabadiliko tunayoyapigania,” Traore amesema katika hafla hiyo siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya nchi hiyo.





