Vijana waanzisha chama cha siasa nchini kenya, waingia rasmi ulingoni
Eric Buyanza
July 4, 2025
Share :
Chama kipya cha kisiasa kinachoongozwa na vijana kilichopewa jina ‘47 Voices of Kenya Congress', kimeingia rasmi kwenye uwanja wa siasa nchini humo. Hali hiyo inapelekea kuujitokeza sura mpya katika siasa za vijana wa Kenya maarufu kama Gen Z.
Kupitia kauli mbiu yake ‘sauti kila mahali' chama hicho kimedhamiria kuangazia masuala na matarajio ya vijana wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kaimu mwenyekiti wa chama hicho Wycliffe Kamanda chama chenyewe kimejengwa kwenye misingi ya ubunifu, uadilifu na ushirikishwaji wa kila Mkenya bila kuzingatia asili au eneo anakotoka kijana.
Taarifa zaidi zinasema, wamepata usajili rasmi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na sasa wako kwenye kampeni ya kitaifa wakiwahimiza vijana kujiandikisha kama wapiga kura na kujihusisha kisiasa.
Hatua hii inaleta mwelekeo mpya katika siasa za Kenya.
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa upinzani wameonyesha kuunga mkono wimbi la vijana na kutumia ushawishi wao.