Vikao vya uteuzi wa Wagombea CCM vyapigwa kalenda.
Joyce Shedrack
July 19, 2025
Share :
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa taarifa ya kuahirishwa kwa vikao vya chama kitaifa vilivyopangwa kufanyika kati ya Julai 18 hadi 19, mwaka huu.
Taarifa imebainisha kuwa vikao hivyo vimeahirishwa hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine kutokana na tatizo la kiufundi lililojitokeza.
Vikao hivyo vilipangwa kufanyika kwa ajili ya kufanya mchujo wa wagombea watakaokwenda kupigiwa kura za maoni na wanachama wa CCM kwenye majimbo pamoja na kupitisha wagombea wa Ubunge wa Viti Maalum kwa makundi mbalimbali na wagombea wa nafasi za Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Zanzibar.