pmbet

Vikosi vya Urusi vimelikamata eneo la Yasnobrodivka

Eric Buyanza

July 9, 2024
Share :

Wizara ya ulinzi ya Urusi imefahamisha kwamba,vikosi vya nchi hiyo vimedhibiti eneo la makaazi la Yasnobrodivka, katika mkoa wa Donetsk huko mashariki mwa Ukraine. 

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters lililochapisha taarifa hiyo, limesema halikuweza kuthibitisha kuhusu taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya ulinzi ya Urusi. 

Ripoti pia zinasema katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, shughuli za uokoaji katika hospitali ya watoto iliyoshambuliwa kwa kombora na Urusi, zinaendelea kwa siku ya pili,huku idadi ya waliouwawa ikitajwa kufikia watu 42.

Takriban watu 200 wengine walijeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya miji kadhaa ya Ukraine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet