pmbet

Vin Diesel yamkuta kama ya P. Diddy

Eric Buyanza

December 22, 2023
Share :

Nyota wa Filamu za Fast & Furious, Vin Diesel amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya Asta Jonasson, mwanamke aliyewahi kuwa msaidizi wake mwaka 2010.
 

Asta amedai Septemba 2010 wakati wakirekodi vipande vya Filamu ya Fast Five aliitwa chumbani kwa Diesel akiwa peke yake ambapo alifanyiwa ukatili wa kingono ikiwemo kushikwa viungo vya mwili bila ridhaa yake.
 

Katika miaka ya hivi karibuni, mastaa kadhaa wamejikuta katika matatizo tangu kuanza kwa harakati za kimataifa za 'Me Too' ambazo zimeshuhudia watu maarufu wakiadhibiwa kwa unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet