Vincent Kompany aunyatia ukuta wa Liverpool
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany anaripotiwa kutamani huduma ya beki wa Liverpool Joe Gomez ili awe mmoja wa wachezaji wake wa kwanza kusajiliwa akiwa meneja wa klabu hiyo ya Ujerumani.
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, uimara wa Gomez umemvutia Kompany wakati huu ambao anajiwekea mikakati ya kuimarisha safu ya ulinzi ya Bayern.
Kocha aliyeondoka wa Liverpool, Jurgen Klopp alikuwa akimchezesha mchezaji huyu katika nafasi za beki wa kati, kushoto, nyuma, kulia na hata katikati...na hii inaweza kuwa sababu kubwa mwalimu Vincent Kompany kutamani huduma yake.