Vinicius Jr akicheza mpira na watoto wa Kim Kardashian uwanjani.
Joyce Shedrack
August 26, 2024
Share :
Nyota wa Madrid Vinicius Jr siku ya jana alionekana akicheza uwanjani na watoto wawili wa Kanye West na Kim Kardashian kwenye dimba la Santiago Bernabeu kabla ya mchezo wa Real Madrid dhidi ya Valladolid.
Kim Kardashian alienda na wanawe wawili uwanjani huku mtoto wake Saint akipata nafasi ya kuingia uwanjani pamoja na wachezaji wa Real Madrid wakati wanaingia uwanjani rasmi kwa ajili ya kuanza kwa mchezo huo wa ligi.
Kabla ya jana Kim na mwanaye huyo mwenye miaka 8 walionekana wakitembelea kwenye jumba la kifahari la staa huyo wa Brazil lililopo nchini Uhispania.
Ikumbukwe,Siku chache zilizopita Kim Kardashian aliweka wazi kuwa watoto wake wamekuwa wakimpelekea orodha ya wachezaji ambao wanatamani mama yao awe na mmoja wao kwenye mahusiano ya kimapenzi.