Vinícius Jr yupo mapumzikoni Dubai, anatafuna tu Biriani!
Eric Buyanza
November 9, 2026
Share :

Winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Vinícius Júnior, amezua gumzo mitandaoni baada ya picha zake kuenea zikimwonyesha akifurahia likizo yake ya mapumziko katika jiji la kifahari la Dubai.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ametumia mapumziko hayo mafupi kupunguza uchovu kabla ya kurejea kwenye majukumu mazito ikiwemo michezo ya kimataifa inayomkabili akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil.
Akiwa Dubai, Vinícius Jr. ameonekana akitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii, kufurahia fukwe za bahari, na mandhari ya kuvutia ya jangwani chini ya jua la wastani la Falme za Kiarabu.





