Vinicius kujipiga pini Real Madrid hadi mwaka 2030.
Joyce Shedrack
April 23, 2025
Share :
Taarifa kutoka Nchini Hispania zinaripoti kuwa klabu ya Real Madrid imefikia makubaliano na mshambuliaji wake raia wa Brazil Vinicius Junior juu ya kuongeza mkataba mpya wa kusalia ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.

Vinicius ambaye alikuwa anatolewa macho na vilabu vya Saudia Arabia anatarajia kuongeza mkataba mpya wa miaka mitatu kuitumikia Real Madrid mpaka mwa 2030.
Nyota huyo alikuwa anamaliza mkataba wake wa awali june mwaka 2027.