Vita vya Iran vyamkwamisha Msuva kujiunga Stars Morice Aitwa.
Joyce Shedrack
March 24, 2026
Share :
.Kiungo Morice Abraham ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars itakachocheza michezo ya FIFA Series nchini Rwanda 
Morice Abraham amechukua nafasi ya Winga Simon Msuva ambae ameshindwa kusafiri kuja kujiunga na Taifa Stars.
Kocha Mkuu Wa Timu Ya Taifa Miguel Gamondi amethibitisha hilo huku akiweka wazi kuwa mshambuliaji Simon Msuva anayekipiga Nchini Iraq ameshindwa kujiunga na timu baada ya kukosa usafiri wa ndege kutokana na vita inayoendelea kati ya Iran Na Marekani.
“Tulifanya kila liwezekanalo kuhakikisha Msuva yupo kwenye kikosi, lakini haikuwezekana kutokana na hali ilivyo sasa. Tumemjumuisha Morice Abraham ili kuimarisha timu,” amesema Gamondi.





