Vita ya kufuzu nusu fainali ya Muungano cup nani kuibuka mbabe?.
Joyce Shedrack
April 25, 2026
Share :
Mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Michuano ya Muungano Cup unatarajiwa kupigwa leo hii kati ya Yanga na Azam Fc utapigwa siku ya leo katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar majira ya saa 2:15 usiku.
Timu hizo ambazo hazijapoteza (unbeaten) mechi yoyote kwenye ligi mpaka sasa msimu huu zitakutana kwa mara ya tatu msimu huu baada ya kukutana kwenye Kombe la Mapinduzi 2026 ambapo Yanga ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare ndani ya dakika 120 bila kupata mshindi.
Nani atafanikiwa kufuzu fainali ya Muungano Cup siku ya leo?.





