Vita ya kuwania nafasi ya pili, Simba na Azam ipo hivi
Sisti Herman
May 22, 2024
Share :
Baada ya bingwa wa ligi kuu Tanzania bara kujulikana kwa Yanga kutawazwa mapema kuwa mabingwa wa ligi hiyo, vita nyingine iliyobaki hivi sasa ni vita ya kuwania nafasi ya pili kati ya vilabu vya Simba na Azam.
Hizi ni takwimu za timu hizo hadi sasa kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara;
1. Simba
Idadi ya mechi 28
Nafasi ya 3
Alama 63
Magoli ya kufunga 56
Magoli ya kufungwa 25
Utofauti wa magoli ya kufungwa na kufunga 31
2. Azam
Idadi ya mechi 28
Nafasi ya 2
Alama 63
Magoli ya kufunga 56
Magoli ya kufungwa 20
Utofauti wa magoli ya kufungwa na kufunga 36
Endapo timu hizo zitakuwa na alama sawa hadi mechi za mwisho, nafasi ya pili itaamuliwa kwa utofauti wa alama.
Mechi za mwisho za timu hizo;
1. Simba
Nyumbani vs KMC
Nyumbani vs JKT Tanzania
2. Azam
Nyumbani vs Kagera Sugar
Ugenini vs Geita Gold
Je unadhani timu ipi itasalia nafasi ya pili?