Vita ya maneno: Hatimaye Slot amjibu Rooney
Eric Buyanza
February 21, 2026
Share :
Arne Slot amejibu madai ya Wayne Rooney kwamba hana uwezo wa kutosha kuwa kocha wa Liverpool.
Mapema wiki hii Rooney alikaririwa akisema Slot hana uwezo wa kuongoza Liverpool kama alivyofanya Jürgen Klopp.
Alipoulizwa kuhusu maoni hayo ya Rooney, Slot alisema:
"Kulinganisha watu ni jambo ambalo kila mtu ana haki ya kufanya, lakini je, hiyo ni haki kufanya hivyo?
"Sote tuko tofauti, lakini kitu pekee tunachofanana mimi na Jurgen Klopp, ni kwamba wote tumewahi kushinda taji la Ligi”
"Lakini hata hivyo, labda Rooney ndiye pekee mwenye maoni kama haya, na ni mara yangu ya kwanza kusikia, lakini pia ni sawa kusema Jurgen ana kiwango” alimalizia Slot.






