Vita ya siku ya mwisho EPL
Sisti Herman
May 19, 2024
Share :
Ikiwa leo ndiyo siku ya mwisho kwenye ligi kuu Uingereza msimu wa 2023/24, timu 20 zitashuka kwenye viwanja 10 tofauti ambapo zitapiganiwa alama na kujua mbivu na mbichi kwenye vita tofauti kama vita ya Ubingwa, Vita ya kutoshuka daraja, vita ya kugombania nafasi za kucheza michuano ya Ulaya pamoja na vita ya takwimu za wafungaji bora wa msimu.
Vita kuu ya Ubingwa itahusisgha viwanja viwili leo, Emirates au Etihad, ambapo itakuwa kwa mara ya nne mfululizo. Arsenal na pointi zao 86, watashuka uwanjani Emirates kukipiga na Everton, wakati Man City yenye pointi 88, itakuwa nyumbani pia huko Etihad kukabiliana na West Ham United. Mechi zote hizo ni muhimu, huku kila upande ukiomba mabaya kwa mwenzake, ateleze mambo yaende sawa, endapo yeye atashinda mechi yake.
Hizi ni mechi za mwisho za msimu zitakazochezwa leo.
Arsenal vs Everton
Brentford vs Newcastle
Brighton vs Man United
Burnley vs Nottm Forest
Chelsea vs Bournemouth
Crystal Palace vs Aston Villa
Liverpool vs Wolves
Luton Town vs Fulham
Man City vs West Ham
Sheffield Utd vs Tottenham
Mechi zote zinachezwa Saa 12:00 Jioni.