Vita ya vigogo imegeukia rasmi kwenye usajili.
Joyce Shedrack
July 8, 2026
Share :
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi kuwa dirisha la usajili kwa msimu wa 2026/2027 kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC, NBC Championship, First League, Ligi Kuu ya Vijana NBC U20 pamoja na Ligi Kuu ya Wanawake limefunguliwa rasmi.

Dirisha hilo lilifunguliwa Julai 6, 2026 na litafungwa Agosti 15, 2026 saa 5:59 usiku, huku klabu zikitakiwa kukamilisha taratibu zote za usajili ndani ya muda huo.
TFF imesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada wa usajili baada ya Agosti 15, 2026, hivyo klabu zote zinapaswa kukamilisha usajili na uhamisho wa wachezaji ndani ya kipindi kilichopangwa.





