pmbet

Viwanda vya Mercedes-Benz Ujerumani hatarini kufungwa

Eric Buyanza

November 13, 2026
Share :

Kampuni maarufu ya utengenezaji wa magari ya kifahari duniani, Mercedes-Benz, imetangaza kusitisha kwa muda uwekezaji wote mpya katika viwanda vyake nchini Ujerumani. Hatua hii inakuja baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya uongozi wa kampuni hiyo na wawakilishi wa wafanyakazi kuhusu namna ya kupunguza gharama za uzalishaji kushindwa kuzaa matunda.

 

Mjumbe wa bodi anayesimamia uzalishaji, Michael Schiebe, alieleza kuwa gharama za sasa za uendeshaji nchini Ujerumani hazitoi nafasi ya kuendelea kuwekeza. Alibainisha kuwa katika baadhi ya vituo vyake nchini humo, gharama za wafanyakazi ziko juu hadi mara tano zaidi ikilinganishwa na viwanda vyake vilivyoko katika nchi za Ulaya Mashariki. Awali, Schiebe alikuwa ameonya kuwa huenda kampuni ikalazimika kufunga viwanda viwili nchini humo.

 

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi anayeshughulikia rasilimali watu, Britta Seeger, alisema ingawa kampuni ingependa kuepuka kabisa hatua ya kufunga viwanda, hali halisi inawalazimu kuchunguza kwa kina ni viwanda vipi wanamudu kuviendesha. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet