pmbet

Vrane Kuungana na Fabregas na Henry Italia

Sisti Herman

July 1, 2024
Share :

Beki wa zamani wa Manchester United , Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Raphael Varane, 31, ameripotiwa kuwasili Italia kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mabosi wa Como iliyopanda daraja na kama wakifikia muafaka anaweza akasaini mkataba wa kuitumikia.

Msimu jana wakati inapanda daraja, mmoja kati ya makocha wa Como alikuwa kiungo wa zamani wa Barcelona na Arsenal Fabregas na pia Thiery Henry ni mmoja kati ya wamiliki wa timu hiyo.

Varane ambaye mkataba wake na Man United ulimalizika jana, msimu uliopita akiwa na mashetani wekundu hao alicheza mechi 32 za michuano yote.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet