Vyombo vya habari U.S.A vyaungana kususia habari za Trump na Ikulu
Sisti Herman
September 22, 2026
Share :

Vyombo vikubwa vya habari nchini Marekani vimesitisha huduma ya pamoja ya kurusha matangazo ya shughuli za Rais Donald Trump kutoka Ikulu ya White House, baada ya utawala wake kuizuia CNN kushiriki katika mfumo huo wa ufuatiliaji wa rais.
Mfumo huo, unaojulikana kama White House TV Pool, unahusisha ABC, CBS, CNN, Fox News na NBC, ambazo hubadilishana zamu ya kurekodi na kusambaza picha za shughuli za rais kwa vyombo vingine vya habari.
CNN ilikuwa imepangwa kuwa mwakilishi wa TV Pool siku ya Jumatatu, lakini ilizuiwa kutekeleza jukumu hilo.
Baada ya CNN kuzuiwa, ABC, CBS, Fox News na NBC zilitangaza k kurusha matangazo ya shughuli za Rais Donald Trump kutoka Ikulu ya White House, baada ya utawala wake kuizuia CNN kushiriki katika mfumo huo wa ufuatiliaji wa rais.
Mfumo huo, unaojulikana kama White House TV Pool, unahusisha ABC, CBS, CNN, Fox News na NBC, ambazo hubadilishana zamu ya kurekodi na kusambaza picha za shughuli za rais kwa vyombo vingine vya habari.
CNN ilikuwa imepangwa kuwa mwakilishi wa TV Pool siku ya Jumatatu, lakini ilizuiwa kutekeleza jukumu hilo.
Baada ya CNN kuzuiwa, ABC, CBS, Fox News na NBC zilitangaza kuwa hazitatuma timu nyingine kuchukua nafasi yake.
Uamuzi huo umeathiri matangazo ya baadhi ya shughuli za Trump, ikiwemo tukio la uzinduzi wa helipad mpya katika eneo la White House, ambapo watazamaji walikosa matangazo ya kawaida yenye sauti kutoka kwa timu ya TV Pool.
Tukio hilo limetokea baada ya White House pia kuwazuia waandishi wa CNN, MS NOW na Politico kuingia katika eneo la White House.
Vyombo hivyo vitatu vimefungua kesi katika mahakama ya shirikisho, vikidai kuwa hatua hiyo inakiuka haki zao za kikatiba zinazohusiana na uhuru wa vyombo vya habari na mchakato wa kisheria.
Kwa upande wake, Trump ametetea uamuzi huo akisema unalenga vyombo anavyovishutumu kwa kutoa taarifa anazoziona si sahihi, huku utawala wake ukisisitiza kuwa suala hilo linahusu upatikanaji wa White House na si kuzuia uhuru wa vyombo vya habari.
Kesi hiyo sasa iko mahakamani, huku vyombo vingine vya habari vikiendelea kuripoti shughuli za rais.





