pmbet

"Waambieni wanaowatuma watoke hadharani"-Ahmed Ally

Joyce Shedrack

August 18, 2026
Share :

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba @ahmedally_ Ameandika ujumbe kwa mashabiki wa timu yake akiwataka kuacha malumbano ya mtandaoni.
AHMED ALLY ALIVYO TINGA NA SIMBA WAKALI KWENYE TAMASHA LA SIMBA DAY
"Mashabiki wa Simba mnaorumbana kwenye vyombo vya habari wote mnahoja za msingi na wote mko sahihi kwa mitazamo yenu

"Agizo langu : Ni wote kuacha mara moja marumbano hayo ili kuipa klabu utulivu iendelee kupambana na ligi kuu

"Kama mnafanya kwa matakwa yenu basi sitisheni kuanzia sasa na kama ni maagizo basi waambieni wanaowatuma watoke hadharani wazungumze wenyewe ili Dunia ijue wanagombania nini?

"Kwa sasa Wana Simba wote tuunganishe nguvu ya pamoja kupambana na maadui 15 wa ligu kuu ya NBC

"Tunachokihitaji ni furaha na furaha yetu ni USHINDI!!

"MSEMAJI WA TAASISI NIMEAGIZA!!" Ameandika Ahmed Ally.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet