pmbet

Waamuzi Mapinduzi Cup Wafungiwa

Sisti Herman

January 11, 2024
Share :

Baada ya malalamiko mengi ya waamuzi wanaochezesha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024, Kamati ya Waamuzi Zanzibar imetoa tamko huku ikitangaza uamuzi mzito wa kula vichwa vya wawili.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Zanzibar, Waziri Shekha amesema kamati imemfungia mwamuzi wa kwanza msaidizi Yusuf Shombe Issa kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria kwa kuruhusu bao la kwanza la Azam na baadaye Singida Fountain Gate ambayo hayakuwa halali katika mchezo wa robo fainali.

Azam iliandika bao la kwanza kupitia kwa Alassane Diao kwa kichwa akionekana ameotea kabla ya Singida kupata bao la pili lililofungwa na Habib Kyombo akionekana pia ameotea na kufanya matokeo ya mwisho Singida kushinda 2-1 na kutinga nusu fainali.

Mbali na Issa, pia Shekha alisema mwamuzi wa pili aliyefungiwa ni Mohamed Mwadini aliyekuwa mwamuzi wa kwanza msaidizi ambaye aliruhusu bao katika mchezo wa makundi kati ya JKU na APR akidai mpira ulivuka mstari wa goli wakati haikuwa hivyo. Mechi hiyo iliisha kwa APR kushinda mabao 3-1 na kwenda robo fainali ikiing’oa Yanga kabla ya kutolewa na Mlandege katika nusu fainali.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet