"Waamuzi sio kwamba wanashindwa kutafsiri sheria" - Nasri Khalfan
Eric Buyanza
June 5, 2025
Share :
Hizi adhabu za kufungia Waamuzi miezi kadhaa kadhaa zimezoeleka sana Tanzania… Je? kama taifa tumeshafkiria namna ya kufanya kuliepuka ili?
Makosa mengi yanayofanywa na waamuzi nchi hii sio kwamba wana shindwa kutafsiri sheria bali ni makosa ya maksudi.. Mfano juzi Hery Sasii alishindwa kweli kutafsiri zile penalty 3 za Singida au ilikua maksudi?
Mbaya zaidi ata wakifungiwa sio kwamba timu zilizo nyongwa ndio zitafaidika… hii adhabu ya Hery Sasii haiwasaidii chochote Singida
Kuna shida mahala kwenye mpira wetu sio kama waamuzi wana shindwa kutafsiri sheria bali ni maksudi tuu nafkiri wenye Mamlaka wanatakiwa kulichukulia hili hatua hiisio kawaida
Hii hali ina haribu sana taswira ya mpira wetu, Ligi inakosa usawa.
Ameandika @nasrikhalfan_ mchambuzi wa soka kutoka @wasafifm