pmbet

Waamuzi wa Kombe la Dunia kulipwa zaidi ya Milioni 260.

Joyce Shedrack

June 10, 2026
Share :

Waamuzi katika Kombe la Dunia msimu huu wa kiangazi wanaweza kupata hadi dola $100,000 sawa na milioni 262,750,300 , huku bonasi kubwa zikilipwa ikiwa watachaguliwa kuchezesha katika awamu za mwisho za michuano.

Gazeti la Times liliripoti kuwa takwimu hizo, ambazo ni karibu mara mbili ya waamuzi waliolipwa kwenye Kombe la Dunia 2014, zinaonyesha nia ya Fifa ya kuwa na waamuzi wa viwango kutumika kwenye michuano hiyo.

 

Fifa ilichagua waamuzi 52 watakaochezesha kombe la dunia pamoja na waamuzi wasaidizi 88 na maofisa 30 wa VAR ingawa idadi yao imepungua baada ya mwamuzi wa Somalia Omar Abdulkadir Artan kunyimwa kuingia katika mpaka wa Marekani na kurejea Istanbul, alikokuwa amesafiria.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet