pmbet

Waamuzi wa Uingereza wazuiwa kuchezesha mechi za Argentina

Eric Buyanza

July 11, 2026
Share :

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limethibitisha kuwa waamuzi kutoka England, Anthony Taylor na Michael Oliver, hawataruhusiwa kusimamia mechi zozote zinazohusisha timu ya taifa ya Argentina katika Kombe la Dunia kwenye hatua zinazoendelea.

 

Uamuzi huo umeelezwa kuwa unahusiana na tahadhari ya kuepusha mgongano wa maslahi kutokana na historia ya Vita vya Falklands vilivyopiganwa kati ya Argentina na Uingereza miaka 44 iliyopita.

 

Kwa mujibu wa FIFA, uteuzi wa waamuzi wa mechi za kimataifa huzingatia vigezo mbalimbali, huku kigezo kikuu kikiwa ni utendaji wa pamoja wa mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili.

 

Aidha, masuala ya kijiografia, historia ya kisiasa na uwezekano wa mgongano wa maslahi pia huzingatiwa ili kuhakikisha haki na uwazi katika usimamizi wa mechi.

Hatua hiyo ina lengo la kulinda uadilifu wa mashindano na kuondoa uwezekano wa kuzuka kwa mijadala kuhusu upendeleo katika mechi zinazohusisha Argentina.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet